*Adaiwa kusambaza akaunti za watu kwenye mtandao...
*Wateja waijia juu NBC...





Picha juu siku ya ijuma polisi kanzu walipofika kwenye ofisi za gazeti la Mwanahalisi jijini Dar es Salaam
---------------
IJUMAA 18,2008,Tanzania kwa mara nyingine tena imeshuhudia uhuru wa habari ukiminywa.Gazeti la Mwanahalisi lilivamiwa na makachero na kufanya upekuzi kutokana na kile walichoita polisi,“kutafuta akaunti za siri za serikali na viongozi wake.”
Aidha,upekuzi ulifanyika pia nyumbani kwa Mkurugenzi Mtendaji na Mhariri Mtendaji wa magazeti hayo,Saed Kubenea.
Akizungumza na Waandishi wa Habari Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai (DCI),Bw. Robert Manumba,amesema kitendo cha makachero wa Jeshi la Polisi kuvamia na kuipekua ofisi ya gazeti hilo na nyumbani kwa Bw. Kubenea na baadaye kuchukua kompyuta kwa ajili ya kufanya uchunguzi zaidi. ni kutokana na mfanyakazi mmoja wa NBC, Bw. Peter Msaki,kuhusishwa na tuhuma za kuchukua akaunti za watu kwa siri na kisha kuzisambaza katika mtandao.
Kwa mujibu wa Bw. Manumba,Polisi ilipata malalamiko kutoka kwa uongozi wa benki hiyo kuwa baadhi ya akaunti za wateja wake zimekuwa zikisambazwa katika mtandao bila ya wao kuwa na taarifa na kuomba wahusika wachunguzwe yani kubenea na Bw Msaki.kwa mengi zaidi Bofya na Endelea Hapa na Hapa....>>>
No comments:
Post a Comment