Wananchi Vumilieni Shida
-Rais Kikwete
RAIS Jakaya Kikwete,amewataka Watanzania kuwa wavumilivu kutokana na hali ngumu ya maisha inayowakabili kwa sasa,inayosababishwa na kupanda kwa bei ya mafuta duniani.
Rais Kikwete ametoa kauli hiyo katika kipindi ambacho Watanzania wengi,hasa wa kipato cha chini wamekuwa wakilia kutokana na kupanda kwa gharama za maisha.
Rais Kikwete alitoa kauli hiyo jana,wilayani Muheza, wakati alipokuwa akizungumza na wananchi wa wilaya hiyo,ikiwa ni siku ya tisa ya ziara yake ya kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo, mkoani Tanga.
Rais Kikwete alisema kupanda kwa bei ya mafuta,kumechangia kwa kiasi kikubwa kulipuka kwa mfumuko wa bei za bidhaa mbalimbali duniani kote.Alisema hali hiyo pia imechangia kuzorotesha kasi ya ukuaji wa uchumi hasa kwenye nchi zinazoendelea na hivyo watu wenye kipato duni kukabiliwa na hali ngumu ya maisha,hususan katika upatikanaji wa mahitaji muhimu,jambo ambalo aliongeza kuwa hata yeye limekuwa likimuumiza kichwa.Kwa habari hii bofya na Endelea Hapa...>>>>

No comments:
Post a Comment