SALAAM ZA SHUKURANI...
Brigedia jenerali Charles Mayunga Jitenga na familia yake watoa shukurani za dhati kwa ndugu jamaa na margiki wote walioshirikiana nao katika msiba na mazishi ya mpendwa waoIRENE NKAMBA JITENGA(Pichani)aliyefariki tarehe 09/06/2008 kwa ajali ya helikopta Arusha na kuzikwa tarehe 11/06/2008 Bariadi Shinyanga.Shukurani za pekee ziwaendee wafuatao:-
.Amiri jeshi Mkuu na Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Jakaya
mrisho Kikwete.
.Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dr.Ali Mohamed
Shein.
.Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mheshimiwa Dr.Hussein Mwinyi.
. Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Davis Mwamunyange na Maafisa na wapiganaji wote
wa kanda za Arusha,Dar es Salaam,Tabora,Mwanza na Shinyanga.
. Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mheshimiwa Isidory Shirima na Uongozi wote wa Mkoa.
. Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mheshimiwa Jenerali Yohana Balele na Mkuu wa Wilaya
ya Bariadi Ndugu Baraka Konisaga.
. Ndugu,marafiki na majirani wote wa Arusha,Dar es Salaam,Mwanza,Musoma na
Bariadi.
. Maparoko wa kanisa katoliki Sinza na Bariadi.
katika msiba huu tulipata misaada na faraja kutoka kwa wapendwa wetu wengi mno.kwa hiyo, haitakuwa rahisi kuwataja wote bali tunapenda kuwashukuru nyote kwa upendo wenu mkubwa katika tukio hilo zito.
IBADA YA KUMSHUKURU MUNGU PAMOJA NA KUMWOMBE MAREHEMU IRENE ITAFANYIKA KWENYE KANISA KATOLIKI SINZA TAREHE 20/06/2008 SAA 5 ASUBUHI BAADAYE KUTAKUWA NA CHAKULA CHA MCHANA NYUMBANI KWA BRIGEDIA JENERALI CHARLES M.JITENGA SINZA KUANZIA SAA 7 MCHANA.
RAHA YA MILELE UMPE EE BWANA NA MWANGA WA MILELE UMWANGAZIE. APUMZIKE KWA AMANI.
AMINA.
No comments:
Post a Comment