Friday, July 4, 2008

NBC yamwaga mkwanja wa tuzo
Mkuu wa Hazina wa benki ya NBC Lawrence Mafuru (shoto) akimkabidhi mwenyekiti wa CTI Reginald Mengi mfano wa hundi ya shilingi milioni 10 ambayo benki hiyo imetoa leo asubuhi kama zawadi ya tuzo ya mtengenezaji bora wa bidhaa wa mwaka.



NBC yafadhili Tuzo ya Rais kwa Mtengenezaji Bora wa Bidhaa wa Mwaka

*Yatoa shilingi milioni 10 kwa CTI
*Yaendelea kusaidia sekta ya viwanda
*Yaendelea kuboresha huduma kusaidia wateja wa kibiashara

Dar es Salaam,
Alhamisi
Julai 3 2008:


Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) kama mmoja wa wafadhili wa “Tuzo ya Rais kwa Mtengenezaji Bora wa Bidhaa wa Mwaka” zitakazotolewa baadaye mwezi huu, leo imekabidhi hundi yenye thamani ya Shilingi Milioni 10 kwa Muungano wa Viwanda Tanzania (CTI). Makabidhiano hayo yalifanyika jijini Dar es Salaam kwenye mkutano na waandishi wa habari.

“Kwa miaka mitatu mfululizo NBC imekuwa mmoja wa wafadhili wa Tuzo ya Rais kwa Mtengenezaji Bora wa Bidhaa wa Mwaka ambazo hufanyika kila mwaka. Kwa mara nyingine tena NBC inayo furaha ya kupewa heshima ya kuwa sehemu ya tuzo za mwaka huu”, alisema Mkuu wa Hazina wa NBC, Lawrence Mafuru wakati wa sherehe fupi ya kukabidhi hundi hiyo kwa Mwenyekiti wa CTI Bw. Reginald Mengi.

Aliendelea kusema, “Kama moja ya benki zinazoongoza Tanzania, NBC inaelewa umuhimu wa kuendeleza na kukuza mazingira ya biashara katika sekta ya viwanda. Hii ndiyo sababu sisi NBC tunaendeleza juhudi za kuboresha bidhaa na huduma zetu za kifedha kusaidia hitaji hili kwa kushirikiana na wenzetu katika biashara. Ni kwa sababu hii pia NBC mwaka jana ilianzisha Vituo vya Biashara kwa makusudi ya kuwapatia huduma wateja wetu wa kibiashara wengi wao wakiwa katika sekta ya viwanda”.

Leo NBC ina Vituo vya Biashara sita vilivyopo kwenye matawi yetu yetu ya Arusha, Mwanza, Tanga, Morogoro, Zanzibar na Kituo Kikuu cha Biashara kilichopo kwenye tawi letu la biashara jijini Dar es Salaam.

Vituo vya Biashara vya NBC vilianzishwa mahususi kwa ajili ya kuendana na kasi ya ukuaji wa sekta ya biashara nchini ambayo imekuwa ikiongezeka katika miaka michache iliyopita. NBC sasa inatoa huduma za kitaalamu zaidi kwa wateja wake kama sehemu ya azma yake ya kuboresha huduma zake.

NBC inaelewa thamani ya wateja wake na zaidi inatambua umuhimu wa Tuzo ya Rais kwa Mtengenezaji Bora wa Bidhaa wa Mwaka kama njia mojawapo ya kuenzi ufanisi mkubwa uliopo katika moja ya sekta kuu zinazochangia uchumi wa Tanzania.

“Tuzo ya Rais kwa Mtengenezaji Bora wa Bidhaa wa Mwaka zimewapa wamiliki wa biashara, Wakurugenzi Watendaji, Wakurugenzi Wakuu na Mameneja sababu ya kujivunia kwa jinsi ambavyo mchango wao unatambuliwa. NBC inawapongeza watengenezaji wote wa bidhaa nchini kwa kutengeneza bidhaa zenye viwango vya juu. Tunaihakikishia sekta ya viwanda nchini kuwa NBC inaendeleza juhudi kubwa ya kushirikiana nanyi kwa kutoa huduma na bidhaa bora zaidi. Tunawatakia washiriki wote wa tuzo za mwaka huu mafanikio”, alisema Mafuru.

Kwa mawasiliano zaidi:
Nector Pendaeli-Foya,


Communication Consultant,


NBC,




+255 754 210903



Mabhe Matinyi,


Media Relations,


Silver Bullet,


info@ayr.co.tz

+255 712785695

Kuhusu NBC
NBC ni moja ya benki inayowakilisha shughuli za kibenki nchini kwa muda wa miaka 40 katika kutoa huduma za kifedha. NBC mbali na kutoa huduma za kibenki za kawaida pia inajivunia yenyewe kwa kuweza kuongeza matawi na wigo wake kwa ukubwa zaidi. NBC inategemea kuwa na matawi 53, mashine 200 za kutolea fedha (ATM) na vituo 197 vya mauzo kwa mpangilio bora nchini kote kwa kufikia mwishoni mwa mwaka huu. NBC imetoa ajira kwa wafanyakazi zaidi ya 4000.

No comments: