Friday, July 18, 2008

Mr Paul: Muziki umenipa kazi
Nchi za Watu..
Kwa mtu yeyote ukimuuliza mafanikio hasa kwa vijana atakwambia nimejenga, nina gari au kitu chochote cha thamani, lakini mtazamo wa Paul Mbenna A.K.A Mr Paul (kama alivyozoeleka na wapenziwa muziki na burudani ) kuhusu mafanikio yake kimuziki anazungumzia elimu, ungana nami kwenye mahojiano na Mwanamuziki huyu kujua ni jinsi gani muziki umemsaidia kimaisha na mtazamo wake kuhusiana na sekta ya muziki hasa wa kizazi kipya nchini mwetu.
Mr Paul kwa sasa anaishi nchini Australia akiwa anafanya kazi jijini Melbourne kwenye taasisi ya Aboriginal an Torres staight Islander Health kama Program Coordinator.
Spoti na Starehe ilipata wasaa wakuhojiana machache na Mr Paul has baada ya kuwa kimya kwenye nyanja nzima ya muziki na kutaka kujua mawili matatu toka kwake,Yuko wapi anafanya nini katika shughuli za kimuziki na kimaisha kwa ujumla,ungana Spoti na Starehe www.spotistarehe.wordpress.com kwa maswali na majibu na Mr Paul.

No comments: