celtel yamwaga zawadi kwa washindi wa Celtel Africa Challenge
Meneja wa Huduma za Jamii wa Celtel Tanzania, Tunu Kavishe (kushoto) akikabidhi hundi ya sh. 600,000 kwa Ofisa Ushirikiano wa Chuo Kikuu cha St. Augustine cha Mwanza, Dk. Bernard Mfumbusa, mjini Mwanza hivi karibuni kutokana na timu ya chuo hicho kushiriki mashindano ya kitaaluma ya Celtel Africa Challenge ya vyuo vikuu yaliyofikia tamati Kampala, Uganda. Mashindano hayo pia yalishirikisha vyuo kutoka nchi za Kenya, Uganda, Malawi, na Zambia.
Meneja wa Huduma za Jamii wa Celtel Tanzania, Tunu Kavishe (kushoto) akikabidhi hundi ya sh. 600,000 kwa kocha wa Chuo Kikuu cha St. Augustine cha Mwanza, Dk. Stephen Barrack Otieno hivi karibuni jijini Mwanza kutokana na timu hiyo kushiriki mashindano ya kitaaluma ya Celtel Africa Challenge ya vyuo vikuu yaliyofikia tamati Kampala, Uganda. Chuo Kikuu cha Engbert cha Uganda kiliibuka mshindi wa mashindano hayo yaliyoshirikisha pia vyuo kutoka nchi za Kenya, Malawi, na Zambia, na kupata zawadi anuwai zenye thamani ya dola 50,000.
Meneja wa Huduma za Jamii wa Celtel Tanzania, Tunu Kavishe (kushoto) akikabidhi hundi ya sh. 600,000 kwa mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha St. Augustine cha Mwanza, Vincent Mihambo mjini Mwanza hivi karibuni kutokana na timu ya chuo hicho kushiriki mashindano ya kitaaluma ya Celtel Africa Challenge ya vyuo vikuu yaliyofikia tamati Kampala, Uganda. St. Augustine ilitolewa hatua ya kwanza ya mtoano ya mashindano hayo yaliyoshirikisha vyuo kutoka nchi za Kenya, Uganda, Malawi, na Zambia.
Meneja wa Huduma za Jamii wa Celtel Tanzania, Tunu Kavishe (kushoto) akikabidhi kombe la fulana kwa Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Augustine cha Mwanza, Mchungaji/Dk. Charles Kitima mjini Mwanza hivi karibuni kutokana na timu ya chuo hicho kushiriki mashindano ya kitaaluma ya Celtel Africa Challenge ya vyuo vikuu yaliyofikia tamati Kampala, Uganda. Mbali na fulana na kombe, pia chuo hicho kilipata hundi ya sh. milioni 6.Picha kwa hisani ya mpiga picha maalumu
No comments:
Post a Comment