BREAKING NEWS
POLISI WAVAMIA MWANAHALISI..
Taarifa zilizonifikia hivi punde ni kuwa gazeti la mwanahalisi limevamiwa muda huu na polisi huku wanaendelea na upekuzi ila hatujui wanataka nini.Waliwakuta ofisini ndugu Said Kubenea(Pichani) na Ndimara Tegambwagwe pamoja na mlizi ndugu Mayunga.Wanaendelea na upekuzi na itakumbuka kuwa hawa hawa ndio ambao walimwagiwa tindikali na kesi bado inaendelea japo haijulikani nini hatima ya haya mambo Wamechukua computer ambayo anaitumia pamoja na flash na wameondoka nae kwenda kumsachi nyumbani kwake na hili lilitokana na kuwa polisi hawa wanatafuta nyaraka fulani Kuna amri ya mahakama ya kufanya hivyo?
Taarifa tulizonazo ni kwamba walikuwa wakitafuta nyaraka za benki zilizomuumbua mzee wa vijisenti na kumfanya ajiuzulu hali inayowafanya waingie kiwewe labda na wao siku moja haya mambo yatawakumba.La maana ni kuwahi mahakamani(kama inawezekana)nadhani ndio sababu wamevamia leo lakini kama wana search warrant na kama inawapa uwezo wa kwenda kusearch hadi nyumbani.Upekuzi nyumbani kwake unaendelea na sasa haijulikani nini kinafanyika huko kwani simu yake haipokelewi tena.Tutawapa yaliyojiri punde.
No comments:
Post a Comment