Wakulima Mkoani Morogoro
wakopeshwa Matreka..
Pichani Mkuu wa Mkoa wa Morogoro,Meja Jenerali Mstaafu,Said Kalembo,akikabidhi funguo kwa mwanachama wa Saccos ya Lupilo,Wilaya ya Ulanga,Mkoani Morogoro,Wadugu Wadugu, mara baada ya kuzinduliwa kwa Mradi wa ukopeshaji wa Matrekta kutoka Kampuni ya DEMACO ya Mjini Morogoro kwa Msaada wa Benki ya FBME ya Dar es Salaam.--------------
WAKULIMA mkoani hapa wamenufaika na mikopo ya trekta yenye lengo la kufanya mageuzi ya kilimo.Mikopo hiyo imetolewa kwa Vyama vya Ushirika vya kuweka na kukopa( SACCOS) vya tarafa ya Lupilo,Wilaya ya Ulanga na Gairo katika Wilaya Kilosa,Mkoani Morogoro.wakulima hao walipewa matrekta kumi na yamepatikana kupitia Kampuni ya Kitanzania ya DEMACO ya Mkoani hapa kwa msaada wa Benki ya FBME ya Jijini Dar es Salaam.
Akizungumza kabla ya uzinduzi wa mradi wa ukopeshaji wa Matreka jana Julai 12 Meneja wa Fedha na uzalishaji,wa DEMACO,Kassim Kashulwe,alisema mpango huo umelenga kuuwezesha mkoa wa Morogoro kuweza kutekeleza agizo la Rais la kuufanya kuwa ghala la taifa ya Chakula ( FAMOGATA).Katika uzinduzi wa mradi huo,mgeni rasmi alikuwa ni Mkuu wa Mkoa wa Morogoro,Meja Jenerali Mstaafu,Said Kalembo na pia kuhudhuriwa na Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii,Jinsia na Watoto,Lucy Nkya,pamoja na baadhi ya wabunge wa Majimbo ya Mkoa wa Morogoro.Habari hi kwa msaada wa Mdau Msimbe/TSN
No comments:
Post a Comment