Saturday, July 19, 2008

TBL Yailipa Serikali
Bil 173..
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bia Tanzania(TBL)Creg McDugar(kushoto)na aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo,Arnold Kilewo,wakiwa katika mkutano wa wanahisa wa TBL uliofanyika jijini Dar es Salaam jana.
---------
Kampuni ya Bia Tanzania(TBL)imeilipa Serikali kodi ya Sh bilioni 173.3 katika kipindi cha mwaka huu,wanahisa wameelezwa.Akizungumza katika mkutano mkuu wa 35 wa wanahisa wa kampuni hiyo uliofanyika Dar es Salaam jana,Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa TBL, Cleopa Msuya alisema kuwa malipo hayo ni ongezeko la asilimia 17.5 kutoka mwaka jana ambapo TBL ililipa Sh bilioni 147.5.
Msuya alisema kwa upande wa shughuli za kibiashara kwa mwaka 2007/2008 ulikuwa wa ufanisi ambapo mapato kwa hisa yaliongezeka kutoka Sh 209.10 hadi Sh 242.2 kwa hisa.“Bidhaa zilizozalishwa na TBL pamoja na kampuni zake tanzu yalipanda kwa asilimia 7.8 hadi kufikia hektolita milioni 2.7 ambazo zilizalisha faida ya Sh bilioni 113,ikiwa ni ongezeko la asilimia 16 zaidi ya mwaka uliopita”,alisema.Habari hii na Maulid Ahmed

No comments: