Thursday, July 3, 2008

Ntakwamisha Bajeti ya Miundombinu
-Mkono
Mbunge wa Musoma Vijijini,Nimrod Mkono ambaye ni wa CCM(pichani),ametishia kutoa shilingi kutoka kwenye mshahara wa waziri wa miundombinu kutokana na kile alichodai kuwa ni usanii unofanywa kuhusiana na ujenzi wa barabara kutoka Musoma kwenda Fort Ikoma.
Mkono ambaye alisema kwamba haungi mkono hoja ya waziri,alisema ujenzi wa barabara hiyo umekuwa unawekwa kwenye ilani ya chama tawala tangu mwaka 1975,wakati huo TANU,hadi katika Ilani ya Uchaguzi wa mwaka 2005,lakini hakuna kilichofanyika."Nataka mniambie,Je, mmesahau?"alihoji Mkono na kuongeza "tangu waondoke wakoloni serikali ya TANU na CCM haijafanya lolote.Nitaungaje mkono bajeti hii?"

Alisema barabara hiyo ambayo ilijengwa na wakoloni wa Ujerumani wakati huo,ni la muhimu katika shughuli za uchumi katika Mkoa wa Mara,lakini serikali imeitelekeza na kuwaachia wananchi wailime wenyewe.Mkono pia alipinga kuelezwa kwamba barabara hiyo ni ya kilometa 64,akasema umbali wa barabara hiyo ni zaidi ya kilometa 100."Hivi waziri hajui hata umbali wa barabara hii? Je huu siyo usanii?Je hizi ni maili au kilometa?"

Alisema hakubaliani na hoja ya waziri ya kuifanyia upembuzi yakinifu barabara hiyo,kwani kwa miaka yote barabara hiyo imekuwa ikiwekwa katika ilani za chama tawala kwa ajili ya kujengwa na siyo kufanyiwa upembuzi yakinifu."Kule Mara kuna Baba wa Taifa amelala.Lakini serikali imetusahau kwenye ujenzi wa barabara na uwanja wa ndege.Mnataka wananchi wa Mara wapeleke mazao yao wapi?Waziri nataka maelezo ya kina la sivyo nitaondoa shilingi kwenye mshahara wako,"alisisitiza.Habari na Msimbe Lukwangule

No comments: