Thursday, July 17, 2008

FC BONGO yaanza kwa mkwara helsinki
FC BONGO YA HELSINKI, FINLAND

Timu ya F.C.BONGO ya Helsinki leo hii katika mechi yao ya kwanza ya Prevention Cup Helsinki imeweza kuwabwaga mabingwa watetezi wa kombe hilo SIERA LEONE bao 2-1 na kujipa matumaini makubwa ya kuendelea vizuri katika michuano hiyo ambayo yanashirikishwa na timu za mataifa mbali mbali.
Vijana hao wa F.C.BONGO watajitupa tena uwanjani siku ya jumapili kwa kuchuana na CONGO na jumanne watakumbana na NIGERIA Kabla kukutana na GREECE alhamisi na kumalizia na ALGERIA jumatatu.

Mabao ya F.C.BONGO yalifungwa na John Ndembo na Ali Apepe.

Ujumbe kwa wana kilimanjaro Stockholm, mnaambiwa kaeni mkao wa nanihii. Chinja chinja wanakuja huko mwezi ujao.

No comments: