Monday, July 21, 2008

Askari Kanzu Saba
Sita ....
Askari kanzu maharufu mkoani Morogoro Patrick Kimaro(Saba Sita)akionyesha kwa waandishi wa habari baadhi ya silaha walizotumia majambazi wakati wakitaka kuvunja benki ya NMB Wilayani Kilombero.ambapo katika tukio hilo watuhumiwa wa ujambazi sita waliuwawa na wengine wawili wanashikiliwa na polisi wakati mmoja alifanikiwa kukimbia.
---------
Na Eline Shaidi,
Morogoro.
MMOJA kati ya watuhuhiwa wawili wa ujambazi wanaoshikiliwa na jeshi la polisi Mkoani Morogoro kwa tuhuma za kutaka kupora fedha katika benki ya NMB tawi la Kilombero,alikuwa ni Mtumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu, imedaiwa.

Hayo yameelezwa na Kamanda wa Polisi Mkoani hapa Thobias Andengenye wakati akiongea na ofisini kwake.Andengenye alimtaja Mtuhumiwa huyo kuwa ni Mwichande Mwinkindo (41) ambaye ni Mkazi wa Kimara B Jijini Dar es salaam,katika tukio hilo alikuwa ni dereva wa gari aina ya Toyota Hilux Pick Up,lenye namba ya usajili STJ 6154.

Alisema jambazi hilo,ambalo hivi sasa limeachishwa kazi katika ofisi hizo kutokana na kuhusika na tuhuma zingine za wizi anazokabiliwa nazo,katika kituo cha polisi Mkoani Dodoma.Hata hivyo kamanda wa polisi hakuweza kuweka bayana tuhuma ambazo anakabiliwa nazo jambazi huyo,ikiwa ni pamoja na nyadhifa aliyokuwa nayo wakati akifanya kazi katika ofisi hizo kutokana na maelezo kuwa bado wanaendelea kufanya nae mahojiano zaidi.

Kwa upande mwingine Kamanda Andengenye alisema mpaka hivi sasa miili ya majambazi sita yaliyouwawa jana katika tukio la kurushiana risasi na polisi,bado ipo kwenye chumba cha kuhifadhia maiti kilichopo kwenye Hospitali ya Mkoani hapo.Alisema majambazi hayo bado hayajafahamika majina yao,na hivyo jeshi hilo bado linaendelea na utambuzi zaidi dhidi ya watu hao,ikiwa ni pamoja na kuendelea kufanya uchunguzi zaidi.

Tangu juzi maelfu ya wananchi na wakazi wa Mkoani hapa,wamekuwa wakifika katika chumba hicho cha kuhifadhia maiti kwa nyakati tofauti kwa ajili ya kutambua maiti za majambazi hayo.Majambazi hayo yakiwa na vifaa mbalimbali zikiwemo silaha za moto,yaliuliwa na polisi Mkoani hapa,Julai 19 majira ya saa 7 usiku,baada ya kufanikiwa kuvunja benki ya NMB,na kutaka kupora fedha katika benki hiyo.Hata hivyon waliwahiwa na polisi kabla ya kufanikiwa katika zoezi hilo.Picha na Mpiga picha maalum wa Thisday.

No comments: