Wednesday, June 4, 2008
Najiamini Nipo Safii-Mzee Sumaye.
Frederick Sumaye, aliyekua Waziri Mkuu wa Rais Mstaafu Benjamin Mkapa kwamiaka kumi, leo amemtolea uvivu bosi wake wa zamani,Ben Mkapa kwa kukataakumtetea "kwa mambo binafsi" akisema kama ni utendaji wa serikali, anaaminikia mtu anajua serikali ya awamu ya tatu ilifanya kazi nzuri,lakini wapo watu binafsi mmoja mmoja waliofanya makosa na kwa kuwa wanachunguzwawatahukumiwa kwa makosa yao na si serikali nzima..
Akatoa mfano wa ununuzi wa rada, ujenzi wa barabara, ununuzi wa ndege, uwekezaji na mengineyo kuwa ni mambo ambayo yana manufaa kwa taifa,lakini kupitia maamuzi hayo mema wako watu ambao walifanya uhalifu kama vile kula rushwa na kuhujumu uchumiwatu ambao alisema wanastahili kuhukumiwa kwa makosa yao binafsi baada yakuchunguzwa na kufikishwa katika vyombo vya sheria.
Alipoulizwa kwanini hamtetei Mkapa alisema, "Kama angekua anatuhumiwa kamakiongozi wangu ningemsaidia kujibu, lakini jamani mambo binafsi mimi siwezikumsemea, Kwani mimi ni mtoto wake?... Si alisema kule Lupaso? Naonahakumridhika,mbona hata Bush anaweza kwenda katika ranchi yakekuzungumzia mambo?"Akasema yeye anajiamini kuwa ni safi mbali ya kuwapo maneno machafu dhidiyake,akirejea sababu ya kuzungumza na waandishi jana,alikua mualikwa katika mkutano wa uongozi wa gazeti la Tanzania LEO (Limekufa) ambao ulifika kumuomba radhi kwa habari yao ya kwamba ana trilioni kumi nje ya nchi naakaunti zake zimezuiwa na JK. cheki MWANAHABARI ANAVYOSEMA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment