Mama Kikwete na Siku ya
Watoto wa Afrika...
Jana ilikuwa siku ya watoto na shamrashamra zake hazikuwa za kawaida. Pamoja na kuzungumza adha zinazowakumba watoto na wale waliotelekezwa lakini walifanya mambo yanayopendeza na kujifunza mazuri kama kukabiliana na ukimwi kwa kuangalia sinema mwishoni mwa wiki na pia Wasanii kutoka katika Kituo cha Dodogodogo Center walitoa burudani katika hafla iliyoandaliwa na Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) Dar es Salaam .
Mwenyekiti wa Taasisi ya hiyo Mke wa Rais Salma Kikwete mwenyewe alihakikisha anazungumza na watoto waliohudhuria sherehe za Siku ya Mtoto wa Afrika zilizofanyika kwenye viwanja vya taasisi hiyo.Picha ni kwa hisani ya Athumani Hamisi na Victor Berege.
No comments:
Post a Comment