Saturday, June 28, 2008

hakuna kabila la wachagga
Kadidi na wadau,
Blog hii ya jamii kwa sasa inaendelea kujadili mada nzito ambazo zinawasaidia wadau mbalimbali katika maisha yao ya kila siku.
Mimi leo naleta mada inayohusu kabila liitwalo 'Wachagga' na kama kweli lipo kihalani. Kwa kuanza naomba wasomi, wana zuoni, na hao waitwao wachagga wawe ndo wachangiaji wakuu katika maelezo nitakayotoa hapa chini.
Ni ukweli kwamba kabila lolote linaundwa na watu ambao wanazungumza lugha moja, na kuwa na mila na desturi zinazofanana.
Kwa kimombo "A CERTAIN TRIBE IS MADE UP OF PEOPLE WHO SPEAK THE SAME LANGUAGE, AND ALSO SHARE THE SAME CULTURES AND TRADITIONS.'
Sasa kwa hawa wanaojiita wachaga waishio mkoani Kilimanjaro wengi wao hawazungumzi lugha moja na mila na desturi zao ni tofauti.
Mfano ni kwamba Warombo wana lugha yao na tamaduni zao tofauti. Hali ni kama hiyo hiyo kwa watu wa Vunjo(watokao Mamba, Mwika, Marangu, Kilema na Kirua, Old Moshi, Uru, Kibosho, Machame, Lyamungo, na Sanya Juu).
Wote hawa wana mila, desturi, na tamaduni zao TOFAUTI. Sasa ni kwa nini wote hawa kwa wingi wao waitwe 'WACHAGGA?'.
Makabila mengine nchini kila moja yana lugha moja, ikiwa ni pamoja na desturi na mila zisizotofautiana miongoni mwa watu.Kwa sasa najitahidi naandika kitabu kuonyesha kuwa hakuna kabila liitwalo
WACHAGGA, bali kuna warombo, wakibosho, wamarangu, wamachame, wauru na wa old moshi. Wadau nipo sawa? Naomba michango...
DEO MUSHI
DAILY NEWS - ARUSHA OFFICE

No comments: