Monday, June 30, 2008

Fedha za EPA zirudishwe
Benki Kuu-Pinda..
Waziri Mkuu,Mizengo Pinda akijibu hoja mbalimbali za Wabunge wakati akihitimisha mjadala wa Hotuba ya Bajeti ya ofisi yake kwenye ukumbi wa Bunge mjini Dodoma,Juni 27,2008.Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu.
------
WAZIRI Mkuu wa Tanzania, Mizengo Pinda,amesema mabilioni ya fedha yaliyoibwa katika Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA),kutoka Benki Kuu (BoT) ambayo ni taasisi ya umma lazima kurejeshwa pasipo mjadala.

Kauli ya Pinda imekuja wakati kukiwa na mjadala kuhusu nani hasa mmiliki wa fedha hizo, kufuatia Waziri wa Fedha na Uchumi Mustafa Mkulo,kusema fedha hizo si za BoT wala serikali bali ni za wafanyabiashara.

Akifanya majumuisho ya hotuba yake mjini Dodoma ,Pinda alisema anajua shauku iliyopo ni kubwa kwani wananchi wengi wanataka kujua fedha hizo ni za nani na mwisho wake ni upi, lakini kubwa ni kwamba fedha hizo lazima zirudishwe kwa gharama yoyote.Habari na Kizitto Noya,Dodoma na Tausi Mbowe.

No comments: