Wednesday, June 25, 2008

Lady jayDee ndani ya UK
LADY JAYDEE aka BINTI MACHOZI NDANI YA UK!!! YUKO TAYARI KWA
SHOO KABAMBE NDANI YA READING JMOSI YA TAREHE 28/06/08
FACE CLUB RG1 7JF NA KUITAMBULISHA SINGLE YAKE MPYA "UKO JUU" KWA MARA YA KWANZA NDANI UK SHOO NI MOJA TU!PICHANI AKIWA NA WADAU WA BONGODJs
------------
Akiwa huko Lady Jaydee atajumuika na masupastaa wengine 15 toka dunia nzima, kumuimbia mandela.. jide ataungana na papa wemba na artists wengine wa2 toka africa kwa wimbo maalum wa sherehe hiyo iltakayoongozwa na marafiki wa mandela will smith na oprah katika shoo itayofanyika siku ya ijumaa juni 27.

Mara baada ya shoo hiyo siku ya pili yake, yaani Jumamosi Juni 28, Jide ataingia Reading kwa shoo moja maalum katika ukumbi maarufu wa FACE CLUB RG1 7JF NA KUITAMBULISHA SINGO YAKE MPYA "UKO JUU" KWA MARA YA KWANZA NDANI ya UK.
Habari zinasema Jide pia ataenda nyumbani kwa mdau Baraka Msiilwa wa Twanga Pepeta kusonga ugali kwa spinachi,dagaa,harage la nazi.. wadau wa ukerewe mnakaribishwa kujilamba maana jide anayo sifa ya mapishi..

Katika shoo ya reading jide ataweka bayana albam yake mpya ya shurkani, ambayo wimbo wake wa 'siku hazigandi' umemuweka katika category tatu za Tz music awards mwaka huu ... best female artist,song of the year na best song writer... upo hapo???

Jide atatambulisha singo mpya ambayo haijatoka bongo, yaitwa 'Uko Juu'.ataitoa ktk ring tone mwezi julai halafu ndio itaenda redioni. humo amewapa mashavu watu wote walio na sifa nzuri ktk fani zao.. jk,DC wa tegeta,mengi, chifupa (rip),sir kim,kaseja na wengine kibao wamo..
ZIARA YA JIDE YA HUKO READING INAANDALIWA NA BONGODJS
NENDA www.bongodjs.com

No comments: