Saturday, June 28, 2008

NMB yazindua huduma za kulipia LUKU kwa ATM

Mkurugenzi Mtendaji wa NMB Ben Christiaanse akiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO Dk. .Idrisa Rashid wakati wa uzinduzi wa NMB ATM LUKU Recharge.

Siku ya Tarehe 25 June 2008, NMB imeweka historia mpya katika utoaji wa huduma za kibenki kwa kuanzisha huduma ya kununua LUKU kwenye ATM za NMB yaani NMB LUKU RECHARGE bila gharama yeyote ya ziada . Huduma hii inaenda sambamba na ukuaji wa uwekaji wa ATM nchi nzima.

NMB ilikuwa ni benki ya kwanza kutoa huduma za kuchukua fedha kwenye ATM bila gharama.Hadi sasa NMB ina ongoza kwa kuwa na ATM nyingi kuliko benki nyingine, hadi sasa tayari ina mashine za ATM 115 na ifikapo mwisho wa mwaka huu itakuwa na ATM 200 nchi nzima.
Chini ni bosi wa masoko wa NMB Imani Kajura (shoto) akipeana mikono na mmoja wa wateja wa kwanza wa Tanesco waliotumia huduma hiyo mara tu baada ya kuzinduliwa

No comments: