mwakyembe amwaga cheche bungeni leo
mbunge wa kyela mh. dk. harrison mwakyembe ametoka kumwaga cheche bungeni sasa hivi, wakati akichangia hotuba ya bejeti ya ofisi ya waziri mkuu, kwa kutoa rai kwamba swala la ufusadi wa EPA ufikie tamati kimoja.
kwa ufupi kasikitishwa sana na kile alichotaja kama maneno kibao yanayosemwa nje ya bunge, mengine yenye lengo la kujisafisha, kuhusiana na ufisadi huo, na kuomba wote ambao hawakupata nafasi kujieleza wakati ule baada ya kamati teule kutoa ripoti yake, wasimame na wajieleze hapo na sio kuzungumzia nje ya hapo.
ametanabahisha kwamba endapo kama katika kujieleza huko hao wanaotakiwa kusema wataweza kudhihirisha kwamba kamati teule haukuwa sahihi basi memba wote wa kamati hiyo wako tayari kujiuzuru.
aidha amesema endapo kamati itapewa muda tena wa kuelezea kila kitu na kudhihirika kwamba wahusika hao wanahusika moja kwa moja basi wao (wahusika) wajiuzulu nyadhifa zao zote.
hii, amesema, ndiyo itakayowezesha mada nyeti ya EPA kufikia tamati na watu kuendelea na mambo mengine muhimu....
No comments:
Post a Comment