Monday, June 9, 2008

Kesi ya Zombe Yaendelea

*Silaa zilizotumika zawasilishwa
Mahakamani

Pichani Silaha zilizotumika katika mauaji ya wafanyabiashara zikiwa mahakamani jana kama kielelezo.
-------
BUNDUKI mbili zinazodaiwa kutumiwa na polisi wanaotuhumiwa kuwaua wafanyabiashara wa Mahenge zimewasilishwa mahakamani .Silaha hizo zilizokabidhiwa jana katika mahakama hiyo, zote ni bunduki aina ya SMG namba 13059192 na 3N0199P.
Shahidi namba 22 katika kesi hiyo, Mrakibu wa Polisi, Juma Bwire kutoka Makao Makuu ya Upelelezi Kitengo cha Uchunguzi wa Silaha, aliieleza mahakama kuwa baada ya silaha hizo kutumika, zilipelekwa kwake zikiwa pamoja na maganda tisa ya risasi.

No comments: