Monday, June 9, 2008
KCMC ni India ya Wanyonge -Mrema
MWENYEKITI wa Chama Cha Tanzania Labour (TLP)Augustine Mrema,amelazwa katika Hospitali ya Rufaa ya KCMC tangu Jumanne,wiki hii akisumbuliwa na homa ya mapafu.Huku akiwa amelala kitandani,alisema katika siku chache alizolazwa KCMC kwa ajili ya matibabu amebaini kuwa uongozi mzima wa hospitali ya KCMC,madaktari na wauguzi wanafanya kazi ya kutoa huduma usiku kucha hali ambayo inatakiwa iungwe mkono na serikali.
Mrema akizungumza na Mwandishi Ally Sonda,alionesha kukerwa na tabia ya serikali kuwasafirisha viongozi wake kwenda nje ya nchi hususani India kwa ajili ya matibabu ambayo yangewezekana kutibiwa na Madaktari bingwa wa KCMC au Hospitali nyingine za hapa nchini na kuongeza hospitali hiyo ya Kcmc Moshi ni India ya Wanyonge.Habari hizi zimetoka Ally Sonda wa Mwananchi Moshi
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment