Friday, March 5, 2010

Mkuu wa Huduma na Bidhaa wa kampuni ya simu za mikononi ya Zantel Bw. Brian Karokola (kushoto) akitoa ufafanuzi wa Ofa mpya ya huduma ya simu za mkononi na mezani kwa gharama nafuu iitwayo “Ofa ya simu za Gumzo”, kwa lengo la kupunguza gharama za kupiga simu kwa wafanyabiashara wadogowadogo na matumizi ya nyumbani . Kulia ni Meneja masoko wa kampuni hiyo Bw. William Mpinga.Picha na Aron Msigwa
Kampuni ya simu ya Zantel imezinduwa ofa mpya na nafuu iitwayo ‘Ofa ya Simu za Gumzo’ kwa simu za mezani na za mkononi kuwawezesha wateja wa Zantel kuongea zaidi ndugu zao walio nyumbani na kuendesha biashara zao kwa unafuu. Ofa ya Simu za Gumzo, kwa mara ya kwanza, inahusisha simu ya mezani au simu ya mkononi na ina viwango 3 vinavyotumika kwa siku, kwa wiki moja au kwa mwezi mmoja.
Akiongea na vyombo vya habari wakati wa uzinduzi wa ofa ya Simu za Gumzo Mkuu wa Biadhaa na Huduma Brian Karokola alisema ofa hii ina nia ya kupunguza gharama ya kupiga simu kwa wafanyabiashara wadogo wadogo na kwa matumizi ya nyumbani. “Tumetoa ofa hii kuwahudumia wateja wenye biashara ndogo ndogo pamoja na matumizi ya nyumbani. Cha muhimu ni kuhakikisha Zantel inatoa mchango wake wa kuhakikisha wafanyabiashara wa wadogo wadogo na wa kati kwa kuwapa viwango nafuu vya kupiga simu kuwawezesha kuendeleza biashara zao kwa gharama nafuu.”
Viwango vya Simu za Gumzo inagharimu shilingi elfu 50 kwa simu ya mezani na shilingi elfu 20 kwa simu za mkononi, na mteja ataweza kuchaguwa viwango 3 kama ifuatavyo: shilingi elfu 1 kutimika siku moja, shilingi elfu 6 kutumika wiki moja na shilingi elfu 20 kutumika mwezi mmoja. Simu zote ya viwango hivi ni za simu za Zantel kwenda Zantel pekee na mteja anaweza kupiga simu muda wowote.
Kujiunga na viwango vya kwanza mteja anatuma ujumbe mfupi wa maneno ZANTEL kwenda namba 1000, kwa viwango vya pili ujumbe ni ZANTEL kwenda namba 6000 na viwango vya tatu ni ujumbe ZANTEL kwenda namba 20000.
“Sote tunafahamu kwamba akina mama wengi wanajishughulisha na biashara na wanatumia muda mwingi mbali na majumbani mwao na kwa kupitia Simu za Gumzo wanaweza kuzitumia sio tu kufanyia biashara bali pia kuwasiliana na wanafamilia waliowaacha nyumbani” aliongezea Bw. Karokola.
Simu za Gumzo pia zinaweza kutumika kupiga simu kwenda mitandao mingine ndani na nje ya nchi lakini itatozwa viwango vya kawaida vya Zantel.

No comments: