Monday, March 8, 2010

Sasa Naridhia Mradi wa Umeme Kupita
eneo la Kanisa Langu-Kakobe



Askofu Mkuu wa Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship (FGBF), Zacharia Kakobe akihakiki vipimo vilivyoko karika mchoro wa mradi wa umeme unaotakiwa kupita katika eneo la kanisa hilo,Mwenge, Dar es Salaam. Mradi huo ulizua utata miezi miwili iliyopita na sasa muafaka unaelekea kupatikana kulia kwake ni waziri wa Nishati na Madini William Ngeleja. Picha na Gloria Tesha
---------
ASKOFU Mkuu wa Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship (FGBF), Zacharia Kakobe, ameridhia mradi wa umeme kupita katika eneo la kanisa lake ambapo amesema atakuwa mjinga endapo atapinga shughuli hiyo ya maendeleo na yenye maslahi ya Taifa.

Sambamba na kuridhia huko kulikoambatana na shukrani kwa Serikali ya Awamu ya Nne kwa kuwavumilia bila kuwapiga mabomu ama virungu, ametoa ombi kwa Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja kuwa Serikali isogeze nguzo za mradi huo mbele zaidi (upande wa barabara) ili athari zisitokee katika kituo cha televisheni anachoratajia kukianzisha.Kwa Habari zaidi Bofya na Endelea....>>>>>

No comments: