Monday, March 22, 2010

hoja ya haja
Tatizo la msongamano wa magari
Dar es Salaam na kwingineko:
Kuingia barabara kuu (Highway intersections)

Naomba nami nichangie mjadala wa tatizo kuhusu msongamano mkubwa ma magari Dar es Salaam ambalo kwangu ni sababu KUU mojawapo ya kupendelea kukaa mikoani na kufanyia shughuli huko.
Na mimi nchi yangu inanisikitish kitu kimoja, kupenda kutatua matatizo wakati wa maafa (crisises?) yakitokea. Tunakaa wee likiharibika ndio twaanza kufikiri. Mengi yamesemwa lakini mimi nitapenda kuchangia sehemu mojawapo ambayo naona haijatajwa (kama imetajwa binafsi sijaona) katika mdahalo huu, nalo ni kuingia kwa magari kutoka barabara za mitaani (ntaita za kitaa) na kwenda kwenye barabara kuu (highway intersection points) na kutoka.

Yametolewa mapendekezo kuwa tatizo ambalo linasababaisha traffic kubwa ni kwenye mataa (traffic lights). Hapa wadau wamependekeza fly overs ili magari yasisubiri (fine). Pia mdau katoa kero inayosababishwa na matuta barabara ya morogoro hususan morogoro road eneo la Stop over na mengine mengi.

Lakini wakubwa huko mipango wanashindwa (Sijui hawataki kufikiri au wanakaa tu kimya makusudi) kutambua ya kuwa barabara kama ya Morogoro au Port access (Mandela kwa sasa nafikiri), pia Bagamoyo (Ali Hassan Mwinyi), na kwa mikoani kama Tanga (niliko na uzoefu nako) ile inayoingia Tanga mjini kutoka mikoani zote hizi ni BARABARA KUU (HIGHWAYS).

Sasa, kama ni highway ni kuwa magari yakipita muda wote yanakwenda kwa spidi angalau ya juu ya Km 80 kwa lisaa na zaidi muda wote. Nafikri kunatakiwa kuwe na kiwango maalumu cha spidi, hususan ya juu. Cha ajabu hapa kwetu hizi barabara zote zina matuta. Tena mengine ni ya kufa mtu!
Nakumbuka siku moja natoa gari Dar bandarini napeleka Tanga, jana yake kumbe waliweka matuta kuingia sehemu moja inaitwa Hale. Ilikua ssa moja moja hivi kigiza kimeingia, yaani we acha tu! vituta viliwekwa vile vifupi ujazo kama saizi ya nguzo za umeme, alafu vipyaa vitatu!!. Na wala kulikua hakuna alama kuwa tuta lipo..pata picha.

Nionavyo tatizo lililo kubwa ni kuwa magari yote yanayotoka katika barabara za ndani (Kitaani) pande zote mbili, kwa mfano, pale Kimara temboni, Suca, mbezi mwisho, pabaya sana ni stopover, zote gari inatoka ndani moja kwa moja inaingia highway gafla! Hii moja kwa moja inaleta foleni na hata kusababisha ajali.
Ukiangalia kwa wenzetu, kwa picha hiyo hapo chini utaona kua gari linapotoka kitaani hata sikumoja haliingi moja kwa moja gafla kama hapa kwetu. Lazima kuwe na ustaarabu wa kuingia ili usimbuguhudhi Yule aliyeko highway na spidi zake lazima aingie kwa spidi yenye kuendana na ile ya highway. Inabidi uchochee kasi ndipo uingie. Hata Yule aliyeko haighway moja kuingia nyingine, lazima aingie kwa spidi ya aliyemo.

Vilevile, kwa magari yanayotoka highway kuingia kitaani lazima kuwe na exits (mitoko) za kistaarabu. Kwa wenzetu unatayrishwa kabisa, kwamba baada ya kilometre moja exit (mtoko) ya kimara inakuja, then unaambaa taratibu kushoto (kwa wale right handed kulia) unatoka zako ndipo unakutana na mataa/traffic lights sasa za kukukaribisha kitaani.
Sisi solution iliyotolewa ni kuweka matuta kabla ya kufika kwenye barabara ya kuingia kitaa. Hii ppia iangaliwe. Zamani mtu ukitoka Tanga unatumia masaa manne kamili kwa basi. Lakini kwa sasa ni masaa matatu mpaka kibaha, na matatu au hata manne mpaka pale Ubungo stendi kutokana na matuta au kusubiri gari lililoko mbele yako liingie kitaa chake mbele. Naona hakuna haja ya kuhamisha stendi mpaka mbezi, ni kurekebisha barabara tu. Wengine watasema ziwekwe double road kila mahala. Sawa, lakini ustaarabu wa kuingia highway lazima uwepo.

Na mikoani kwenye kila kituo, kabla ya kufika matuta yamejaa tele, hakuna hata raha ya kuendesha gari. Ni kosa nafikiri kwa highway kuwa na matuta. Sikuizi miji inapanuka pembezoni mwa highways zetu.
Watu nao wanaongezeka. Basi mtu akigongwa tu wanalala barabarani mpaka waletewe matuta, na ndicho kilichotokea barabara ya Tanga kuanzia Segera. Ilikua kati ya barabara bora kuliko zote kutengenezwa Tanzania, mpaka leo haijaharibika vile. Ni matatuta ndio yameiharibu.
Kama watu wanagongwa (kwanza kusiwe na crossing ya watu kwenye highways) ama wapite juu au chini kwa mpangilio unaofaa. Pia, kwa nini kila kimji kiwe na barabara ya kuingia highway? Kila baada ya kakilometa kuna kakituo pembezoni tu mwa “highway”, ukiongeza na ustaarabu wa daladala wa kuingia na kutoka kituoni kuingia highway nalo tatizo linazidi la foleni na ajali kwani mtu yuko highway basi laingia gafla. Ingefaa vituo vyote view kama cha pale kibaha au ndani zaidi, na kuingia kwao highway waingie kwa kasi inayofaa. Kama vipi tubadilishe maana ya barabara zetu, kama ile ya morogoro, je ni highway au kwa sasa inafaa (qualify) kuwa ya kitaa? Kuanzia kibaha ndio iitwe highway kwa maana ya highway yenye spidi.

Kwa watani wa jadi hapo Nairobi nimeona wamejaribu lakini highway intersection zao ziko very tricky, yaani ni fupi mno. Haimpi mtu nafasi ya kuchochea spidi mpaka kuingia highway hivyo nao bado ajali ni nyingi.

Ila mdahalo wa foleni pia ni mpana na unataiwa kuboresha sehemu nyingi tu, kama kuboresha public transport ili watu wasinunue magari, hii ni mjadala mwingine tena.

Wengine wataboresha haya niliyoandika, mathalani maana, mpangilio na matumizi, hasa ya neno barabara kuu.

Ni hayo tu kwa leo
Mdau Tanga

No comments: