Saturday, March 13, 2010

Aina Mpya ya Ukwapuaji waingia Bongo
----
Ndugu zangu

Kuna tukio limetokea hapa Sinza maeneo ya Mapambano njia ya nyuma
kama unaenda Mwenge kwenye miti mirefu bar moja inaitwa kwa jimmy .

Kuna vijana 2 walikuwa wanatembea njiani mmoja kabeba begi lake la
vitabu ghafla gari ndogo ikampitia kwa pembeni mtu aliyekwepo ndani ya
gari akakwapua begi la yule kijana ambapo kulikuwa na simu na karatasi
zake .

Huyo kijana alipiga kelele kidogo nilikuwa mbele yao nikajua labda ni
tatizo lengine kumbe wenyewe wameibiwa bei lao kwahiyo ile saloon car
nyeupe ikakimbia moja kwa moja

Kijana aliyeibiwa anaitwa Erick Thomas Jongela simu yake anasema
ilikuwa na line 2 moja ni 0715 241204 na 0756 816 770 hizi line
zilikuwa kwenye simu hiyo iliyokwepo kwenye begi lililoibiwa

Mwenzake mwenye simu anaitwa Fadhili no yake ni 0713 76 59 05

Kwa mtindo huu jamani muwe makini mnavyotembea na mabegi yenu pamoja
na mali zingine zisivutie sana wahalifu hawa .

Nimetoa kisa Hichi kama tukio la kweli lililomkuta mtu naamini tigo
pamoja na voda kwa kushirikiana na vyombo vya dola vitaweza kufuatilia
simu ya kijana huyo na kuweza kupata taarifa zingine zinazohusiana na
simu hiyo toka ilipozimwa mara ya mwisho

Mdau

No comments: