Wednesday, March 17, 2010

JAMANI TUJUZANE KATIKA HILI !!
Mkuu habari..
Kuna malipo ya beach parking ambayo tumeana kulipishwa kwa upande wa Coco Beach al-maarufu kama Coco ya wahindi. Yaani siku hizi kuna malipo ya beach parking kwa kila weekend tu.
Ningependa kupata msaada wa kujua kama ni kweli au la wadau wanaibiwa. Kama ni sheria imewekwa na manispaa ya Kinondoni au ni mradi wa wajanja flani. Kama ingekuwa ni sheria ya manispaa mbona beach zote za public hazina parking fees? Na hizo fees zinatumikaje kwani hatuoni lolote linalofanywa hapo mahali kama vile ujenzi wa vyoo na sehemu za kutupa taka na huduma zingine za msingi kwa jamii. Hii imekaaje?
Mdau Ostabei

No comments: