mwenye macho asikie, na mwenye masikio aone...
bwana kadidi2 na wadau wengine,
kwanza napenda kuchukuwa fursa hii kuwashukuru kwa kuwapatia watanzania taarifa mbali mbali za kila siku.
pili napenda kutoa ufafanuzi kuhusu tangazo la kazi nchini saudi arabia ambalo lilitoka katika blog ya jamii. mimi ni mtanzania na ni dereva huku saudi arabia na ninayoeleza hapa ni kuwa naendelea kuyapata ikiwa ni pamoja na mateso, manyanyaso na uonevu uliopindukia mipaka katika ubinaadamu.
kwa ujumla hapo dar kuna magenge mawili yanayofanya biashara ya kuandikisha watu kazi na kuwasafirisha kuwaleta huku saudi rabia. mimi ni mmoja wa walioumizwa na genge moja wapo. wanachukuwa fedha kwa waarabu huku saudia na kuwaahidi kuwa watawapatia madereva. kisha wanatangaza nafasi kama hizo huko nyumbani na wanadai kuwa kila anaetaka kazi alipe nauli, viza, ukaguzi wa afya na gharama nyenginezo. jumla huwa baina ya shs laki 8 hadi milioni moja.
aidha wanadanganya watu kuwa mishahara ni riyal 3000. naomba ndugu zangu nikuelezeni ukweli kuwa hakuna dereva anaelipwa riyal 3000. hata sisi tulidanganywa hivyivyo. huku mishahara ya maredeva ni riyal 500 hadi 800. ukibahatika basi ni 900 ijapokuwa kisheria ni riyls 1300 hadi 1500. lakini hakuna mwarabu anayelipa pesa hizo.
baadhi ya uongo wanaodai hao matapeli ni kusema kuwa riyal ni sawa na dola ya marekani wakati wanajua ni uongo. pia hudai kuwa riyal ni shs 350 (angalia tangazo lako) wakati ni shs 300 tu za tanzania. mbali na udanganyifu huo, hawatoi mikataba kwa madereva au kama wanatoa ni feki na wanapofika huku huambiwa mikataba ile si sahihi na kupewa mikataba mipya. pia tunasainishwa mikataba iliyoandikwa kwa kiarabu wakati sisi hatujui kiarabu.
mimi mwenyewe na wenzangtu tulianza kuzusha vurugu tukitaka kurudi nyumbni na baada ya kudai hivyo, waraabu wakatuletea polisi na kupigwa. isitoshe tukaambiwa kama mtu anataka kurudi basi alipie gharama yote iliyotumika kumleta saudia na ajigharamie nauli ya kurudi huko. kwa ujumla tumeshindwa na tunaendelea na kazi mkataba ukiisha tunarudi bongo.
pia ni uongo kusema kuwa madereva wanapewa nyumba. tunaishi katika magari. gari lako ndio nyumba yako na mabegi ya nguo humo humo. kampuni za huku zina madereva 300 hadi 500. jee wataweza kumpatia kila mtu nyumba?

watu waache kudanganya watanzania. tupo hapa na wapakistan, wahindi, wabengali, waphilipino, wasudan, wanigeria, wakenya na waethiopia. tunaishi maisha magumu sana. sahani ya chaklula ni riyals 45. sasa niambie riyal 800 utaishi vipi? hiyo mishahara huyo jamaa anayodai ni ya wahasibu, madaktari au wahandisi sio madereva.
pia mjue kuwa msaudi katika nchi yake hana kosa. hata ukienda katika vyombo vya sheria huwezi kumshinda. jamaa wana jeuri, kiburi sijapata kuona. tena anakwambia nenda kokote na mwisho utarudi hapa. pia ukufika uwanja wa ndege tu wanakunyanganya pasipoti na huioni tena hadi isku ya kuondoka baada ya kumaliza mkataba. hivyo unakuwa mtumwa huwezi kukimbia wala kufanya lolote.
naomba serikali ituhurumie sisi na hao wanaodanganywa huko tz. ipige marufuku biashara hii ya utumwa maana sisi tunateseka mno. wengine tumeuza viwanja, mafrji, na mali nyenginezo tuje huku lkn maisha sivyo tulivyotarajia. inasikitisha sana.
ubalozi wanajua hali hii, na tukienda kulalamika wanachukua juhudi za kuwasilina na serikali ya saudia lkn waarabu wanateteana. hakuna hatua zozote zinazochukuliwa na serikali kwa raia wao. tunashukuru juhudi za ubalozi lkn hazizai matunda kwa kuwa saudia serikali inawatetea matajiri wanaonyanyasa sisi wageni..
naomba kama haya ni uongo hao wanaodanganywa wapige simu ubalozini kuulizia wasikie watakayoambiwa.

hapa wapo watz wapo jela mwaka mzima sasa wmeshamaliza vifungo na jamaa hawataki kuwatoa. pia wapo wameletwa siku za karibuni nao sasa wanaanza kualamika. kazi masaa 24 ukipata ajali na gari unakatwa mshahara eti kurepair gari wakati gari zote zina bima. wanatuonea sana hawa waarabu. hatuna jumamosi wala jumapili wala sikukuu.
wapo wenzetu waliopata ajali na kuumia basi hawalipwi mishahra eti hawafanyi kazi wakati ajali mtu hakujitakia. naomba serikali iwakamate hawa jamaa wanaotapeli watu huko bongo na kuwasababishia watz mateso huku uarabuni.
ni mimi mwathirika na kazi ya udereva.

No comments:
Post a Comment