Duma anajulikana kwa jina la wa chini kwa kuwa yeye ni mzee wa mbio mbio. Hana ujanja wa kupanda miti kama binamu yake, wa juu (chui). Tofauti kati ya wa chini (duma/Cheetah) na wa juu (chui/leopard) ni kwamba wa juu ana umbo lililojengeka kinamna wakati wa chini yeye ni lightweight - kimbaumbau. Hali hii ndio inayomfanya awe na uwezo wa kutimua mbio na kuwazidi wapinzani wake.
Anapokuwa anakimbia, wa chini hutumia mkia wake kuweza kupata balance akiwa ktk spidi kali. Hii ni muhimu kutokana na hali ya kwamba mwili wake ni mdogo (kimbaumbau). Mkia wake ni nyenzo muhimu sana kwake.
Wa juu hufanya issue zake mida ya mchana na usiku hupumzika (mara nyingi). Kutokana na yeye kuwa ni mnyama anaewinda mchana, pembezoni mwa macho yake kuna rangi nyeusi ambayo kazi yake ni kuweza kumsaidia kuona vizuri akiwa kwenye jua kali. Rangi hii huwa kama sun glasses kwake. Hii ni hali ambayo wanyama wengi wanaofanya shughuli zao mida ya mchana huwa nayo ktk macho yao.
No comments:
Post a Comment