Tuesday, March 30, 2010

hali halisi ya tunduruzzz to daslaam.






Mzee wa libeneke mambo yanakwendaje?
Nimeamua kushiriki kwenye blog kwa kutuma picha na ukiona zinafaa basi utaziweka ili wadau wapate kuziona.Nilikuwa na safari ya toka tunduru hadi masasi na kisha masasi mpaka dar.Nilitoka tunduru ijumaa na kulala masasi wiki iliyopita.
Nimetoka masasi jana j3 kuja dar.Wiki iliyopita watu wamelala sana njiani kati ya Somanga na Muhoro ila jana tumepita bila tabu sana sehemu hiyo ila kuna baaadhi ya matukio ambayo nimeona niyatume baada ya kupiga picha kadhaa.
KAKA KULE KUSINI KWETU MWENZIO AKINASA KWENYE TOPE JARIBU KUSAIDIA ILI ATOKE.UKIJIFANYA UJANJA UANZISHE NJIA YAKO BASI LAZIMA UKAE TENA VIBAYA ZAIDI KULIKO YULE MWENZAKO.
Picha za njia ya Tunduru hadi Masasi zinahusisha basi nililopanda mimi na hizi nyingine zinahusisha malori yaloyoziba njia katika kipande cha kutoka Somanga hadi Muhoro kuelekea nyamwage na hatimaye ikwriri.
Ni hayo tu kaka.
Ni mimi mdau wa Blog ya hii "Joseph"

No comments: