Saturday, March 20, 2010

Kuna sakata la uchafuzi wa mazingira huko Mara




"Kuna sakata la uchafuzi wa mazingira huko Mara...Ilinibidi nisitishe shughuli zangu na kuandika nakala fupi kuwaomba viongozi wetu chonde chonde"!


==== ========== ========== ===========

Kinachotia hasira zaidi ni ukimya wa Serikali yetu na watu wengine husika (uongozi wa Barrick Gold Mine)! Jamani, hawajui haya yanayojiri huko mto Tigithe? Au wamekuwa na roho ngumu kiasi kwamba vitu kama hivi haviwashtui? Hawajali?

Nimeshawahi kusoma visa kama hivi, ambapo urasimu na uchunguzi wa kuhakikisha kuwa takataka kutoka kwenye migodi ndio chanzo cha matatizo kama haya tunayoyaona huchukua miaka.

Bahati mbaya wakati muafaka unapatikana vijiji karibu na Tarime vitakuwa vimesha'angamizwa; na hakuna fidia yoyote - kwa watoto na ndugu zao - itakayoweza kuwarudishia maisha yao!

Jamani, viongozi wetu chonde chonde, jamani! Kwenye usahili wa mgodi huu hamkuangalia vitu muhimu kama utupaji wa takataka za sumu? Au, hata hamkutaka kujua ni aina gani ya takataka zitatoka kwenye mgodi huu? Hela mnazopata ndizo zinawafumba macho?
ASANTENI
VIJANA FM

No comments: