Wednesday, March 24, 2010

Utaipenda uta ipenda !!
yale yaleeeee....
Hivi kweli serikali imeshindwa kabisa kabisa hata kuwa na Domain jamani, kwanini email address za watu wa serikali ni za yahoo, hotmail au gmail??
Hivi elimu hawana ya kuwa kitengo kama cha serikali kutumia free address ni aibu hata kwetu sisi wenye ufahamu wa mtandao , tunaonekana ushauri wetu kwa serikali ni hakuna!!
Embu ankal fanya kila jambo tuwahimize wakubwa huko kufanya mara moja hili la email address. Iweje wawe na website ya taifa washindwe kuwa na email za .go.tz ?

Natumaini utalituma hili kwa walengwa hata basi tulijadili na tulitekeleze, mimi ni mtu wa action zaidi kuliko hizi bla bla bla huwa siziwezi kabisa. Yaani inakera mpaka basi.
Mdau Barabara ya Ocean Rodi

No comments: