Thursday, March 25, 2010

Ajali mbaya imetokea kibamba-kibaha leo

Habari zilizoifikia hivi punde blog hii ni ya kusikitisha sana na pia inaelezwa kuwa ajali mbaya imetokea mapema leo asubuhi barabara ya Morogoro jijini dar maeneo ya Kibamba-Kibaha,inaelezwa kuwa Lori la mafuta limeivaa Hiace iliyokuwa na abiria na kuitumbukiza chini ya daraja na kuilalia Hiace hiyo kwa juu.Mpaka muda huu inaelezwa kuwa abiria wote waliokuwa kwenye Hiace hiyo wamefariki papo hapo,hivyo juhudi za kuondoa maiti eneo la tukio zinaendelea na kwamba magari mawili ya zimamoto yamekwishawasili eneo la tukio.

Tutazidi kuwataarifu zaidi kadiri ya habari zitakavyokuwa zinatujia. ingawaje mpaka sasa sijafika eneo la tukio kuweza kuwapa japo chanzo cha ajali . Yoyote alieko huko anaweza akatujuza.


No comments: