Saturday, March 13, 2010

Temeke Inaongoza Kwa Utajiri Tanzania, Lakini...


Kwa mujibu wa takwimu, Wilaya ya Temeke ndio inayoongoza nchi nzima kwa kukusanya mapato. ( Ina bandari, viwanda, Uwanja wa Ndege, Uwanja wa Taifa na mengineyo). Temeke inafuatiwa na Wilaya ya Kahama yenye madini mengi pamoja na bidhaa za mifugo na kilimo. Temeke kwa sasa ni Wilaya pekee miongoni mwa Wilaya za Mkoa wa Dar es Salaam ambayo haina msongamano mkubwa wa magari. Pamoja na Temeke kuongoza kwa kukusanya mapato, bado Temeke ndio wilaya inayoongoza kwa kuwa na wakazi wengi wenye maisha duni miongoni mwa wilaya za Mkoa wa Dar es Salaam. Nini kifanyike?

changamoto kutoka kwa kaka mjengwa.

No comments: