Saturday, March 20, 2010

Du Hii utaikuta hapa tu Tanzania !!
Risiti ya malipo kwa magari uwanja wa ndege
wa Julius Nyerere International Airport....


Leo bwana mie nimewahi asubuhi 7.15am ili nisafiri na Precision Air ya 9.30am Am,checkin was 7.30 nimekuta ndege flght no PW 730 wamecancel mpaka jioni saa 3pm. Ikabidi nimpigie dreva wangu arudi kunifuata airport. Ah nao Precision basi si wangekuwa na utaratibu japo wa kutuma sms kwa wateja wao kuwajulisha canceletions? Ah hiyo nayo ni hadisi ingine
CHA AJABU-UHUNI WENYEWE
Kuingia na gari airport lazima ulipe Sh 500, hata kama unamshusha mtu/kupokea mtu.imelazimu kulipia mara mbili kunishusha na kunirudia after flight cancelation.uhuni upo pale katika ticket office ya Airport na watu wa gate la kutoka.nimelipa pesa nikapewa risiti ya mkononi,wakati computer zipo na zinafanya kazi,risit imeandikwa Sumbawanga Airport kama picha inavyoonyesha.
katika Exit Gate, nimekuta mtu anapokea ticket hizo na gate likiwa wazi,inakuwaje ukiingia gate linafanyakazi na hupiti bila risit,ila ukishalipa gate la kutoka linakuwa bovu,sasa hapa kuna ujanja na uhuni wa kuhujumu mapato,kwa ulaya,hata kenya and other serious airports, ticket inatoka ktka machine na ukilipa machine inavalidate muda na pesa uliyolipa ndo gate linafunguka.
sasa pesa nimelipa ,ticketi nimepewa ya mkononi kama daladala or parking za dar,mbaya zaidi ni ticket ya sumbawanga (lol) plus amount on receipt ni sh300!!
najua maboss wa wahusika wanapitia hii ,ningependa kupata their views,and kama ikibidi livaliwe njuga na wahusika ili tupewe huduma bora kama wanavyojitangaza. ni hayo tu kwa leo,mdau wa libeneke

No comments: