UCHAGUZI UVCCM
MFAHAMU NAPE MOSSES NNAUYE
-----
MFAHAMU NAPE MOSSES NNAUYE
-----
Ndg Nape ni miongoni mwa UVCCM wachache mno wanaochukizwa na mfumo unaoendeshwa ndani ya umoja wetu wa vijana,na pia ni miongoni mwa wanachama wanaopinga mambo ya kifisadi yanayotokea leo hii ndani ya nchi na chama,tunaamini kabisa mwaka huu Nape,si Nape wa wakati ule,kwani amejiandaa vya kutosha na ana kila dalili za kuwa mwenyekiti wetu wa UVCCM,dalili ambazo zinatumika hata kuwapata marais wa nchi mbalimbali zinazoendelea na zilizoendela.
Nape ni kijana hodari, makini na ni mzalendo haya yote yamejithibitisha kwa nyakati tofauti tokea ameanza kuwa mwanasiasa katika siasa za umoja wa vijana na chama wa ujumla,ameweza kushinda chaguzi za nec taifa mara mbili,hii inatokana na umakini wake,uhodari wake na pia uzalendo aliokuwa nao katika kuhakikisha anakipigania kile anachokiamini,hasa kikiwa ni sahihi na kina manufaa kwa chama na kwa taifa letu la jamuhuri ya muungano wa Tanzania.
Miongoni wa vijana ambao walioshawishi nec taifa kuwa na matawi ya nje yeye ni mmoja wapo kwani kufanya hivyo chama kitaweza kuwa na wanachama wasomi ,ambao wanahitajika kuja kuitumikia nchi katika nyanja mbali,aliliona hili baada ya kuwa nchi imeingia katika mfumo wa vyama vingi vya siasa,na kwa hiyo balozi zetu haziwezi tena kuendesha matawi ya nje kwani mfumo umebadilika na kwa hiyo kuepusha migongano na vyma vingine vya kisiasa alishawishi chama kupitisha katiba ambayo itaruhusu kuwa na matawi ya nje,katiba ilipitishwa leo kuna matawi tele tele huku na kule Uingereza,Urusi,Malaysia,China,India nk,tena mengine ameshiriki kuyasimika kama ya Bangalore,Mysore India....hii inajionyesha wazi kuwa si kijana wa mzaha pindi linapokuja suala lenye maslahi na nchi yake ya Tanzania na chama chake.
ndugu wanauvccm wamarekani watu kama akina Nape huwa wanawaita capital brain,nini maana yake ,maana yake ni kuwa nchi inapofika mahala inahitaji kujiweka sawa katika mambo ya msingi inawatumia watu kama hawa,katika siasa,uchumi,kilimo,biashara,ulinzi,uhusiano wa kimataifa nk,sasa iwaje watanzania wenzangu wana UVCCM tushindwe kumtumia kijana huyu katika fani ya siasa?no let us give him a chance and we shall see the achievement of being using this kind of people.
Wapinzani wameanza kummulika kwa tochi ya aina yake,tumemsikia Mwenyekiti wa TLP akitangaza katika vyombo vya habari na magazeti ya kuwaccm wakimzingua anaweza kwenda upinzani,huyu ni mrema na tunafaham mrema ni miongoni mwa waliokwisha kuwa maafisa usalama huko zamani,mwalimu,pia mwanaccm na waziri katika serikali ya Mzee Mwinyi,katika hili anajua vizuri,huyo ni mrema na je vyama vingine ambavyo vimekaa kimya?japo tunaamini Nape leo hii hawezi kukihama chama chake cha mapinduzi,labda ngamia aweze kupita katika tundu la sindano,kitu ambacho ni kigumu.
Uchaguzi wa mwaka huu wa nec taifa uligubikwa na wimbi kubwa sana la kila aina ya vituko tuvijuavyo,wapo walishapangwa kwamba wao kuingia tena ndani ya NEC wasahau,wapo waliokuwa wamekata tamaa,lakini kijana huyu ni miongoni mwa vijana wachache waliopita huku na kule kuhakikisha hakuna dhuluma au michezo ya kijasusi inachezeka katika uchaguzi,ndio maana leo hii nec taifa iko imara maana ina wajumbe mahodari,makini na wazalendo wanaounda nec imara .
Nape wa leo ni msomi aliyeiva ipasavyo,mwenye shahada ya kwanza inayohusu mambo ya uandishi wa habari na saikologia,ambayo ameipataBangalore University India,(hakusoma kwa njia za internet amekaa india kwa miaka mitatu)si sawa na zile degree,masters au Phd za online(internet),ambazo hazimuwezeshi mtu kuwa ameiva ipasavyo,anastashahada ya diplomasia ya chuo cha kivukoni pia.
Wanauvccm wenzangu, naamini kabisa tunamfaham Nape vizuri, yaliyomo humu ni baadhi ya machache tu ambayo yanamtofautisha na wanauvccm wengine,alipokuwa anagombea kwa mara ya kwanza nafasi ya unyekiti akichuana na Bw Nchimbi aliweza kumpa shida sana mpinzani wake,yaliyojitokeza wakati ule tunayafaham na naamini mengine bado tunayakumbuka nawaomba tusiruhusu yajitokeze tena mwaka huu,wasawahili wanamsemo usemao,..“yaliyopita yamepita tugange ya sasa”.
wagombea mwaka huu ni wengi...wengi na kila mmoja ana mikakati inayomuhakikishia ushindi,kati ya wote waliojitokeza kugombea nafasi mbali mbali,sisi kama wapiga kura hapo december 13/14 ni lazima tujiulize ni wagombea wapi ambao kwa kusema ukweli tukiwatizama usoni wanajieleza kwamba wao wanaguswa na hali ya nchi ilivyo hivi sasa?maana kama kweli tunataka mabadiliko ya kweli ndani ya nchi yetu lazima mabadiliko hayo yaanzie ndani ya uvccm na si kwengineko.
maana ni ukweli usiojificha ,wapo wagombea waliopandikizwa tu kwa ajili ya kufanya lile ambalo waliompandikiza wanalihitaji,huku si kuijenga jumuiya ya umoja wa vijana, bali ni kukididimiza chama kiujumla, ni hatari sana kama wanaUVCCM hatutokuwa makini,Baba wa Taifa mwalimu Nyerere aliwahi kusema katika hotuba zake kwamba upinzani wa kweli ndani ya nchi unaweza tu kutoka ndani ya ccm,na si kwengineko,hili linaweza kutokea tu pale ambapo misingi imara ya chama isipotekelezwa , hili linaweza kujitokeza....nawaomba sana wanajumuiya wenzangu tuwe makini sana tutakapo kwenda katika uchaguzi wetu mwezi december mwaka huu 2008,tusikubali kurudia kosa,"if the solution is simple God is answering.
Imeletwa Na
mtata_mtatuz@yahoo.com
Mjumbe UVCCM .

No comments:
Post a Comment