Wednesday, August 20, 2008

Anga Ya Tanzania Na Kilimanjaro
Yetu..!
Hata ukipanda ndege ya mashaka, anga ya Tanzania bado inaweza kukupunguzia hofu.Nchi yetu ina vijiji takribani elfu kumi, na kila kijiji kina shule ya msingi,na kila shule ya msingi ina uwanja wa mpira,hivyo basi,hata rubani akipata matatizo kwenye anga ya Tanzania,ni rahisi sana kwake kutua kwa dharura kwenye uwanja wa shule ya msingi kwenye moja ya vijiji vingi vya nchi hii.
Na kwa vile shule nyingi hazina mipira ya kuchezea,ni aghalabu rubani akawakuta watoto wakicheza mpira uwanjani!Pichani ni mlima Kilimanjaro jana mchana.Watani zetu wa jadi (Kenya)wamefaulu kuutangaza mlima huo kuwa uko kwao na wanachuma pesa kwa mlima wetu!
Na mdau
Maggid Mjengwa

No comments: