Friday, August 29, 2008

Tunaomba msaada wa kumtafuta huyu
"Mzee Utamu'

---------
Ndugu
MICHUZI,JIACHIE,TZUK,MJENGWA,KADIDI NA HAKINGOWI

watanzania wote wa kila pande za dunia wanakufuraia kwa kuanzisha mtandao wenye habari motomoto za kote duniani na tukiangalia namba ya watanzania wanaoingia katika blog yako ambao karibu wanafika millioni 5 hiyo inaonyesha ni jinsi gani ya kazi nzuri unayo ifanya. tunakushukuru saana.

Tatizo kuna mtu tumeanza kumtafuta na tunaomba wananchi na watanzania wema,wastaarabu wajitokeze na kutuambia huyu mwenye blog ya utamu ni nani ? na anaishi mji gani? ili hatua za kisheria zichukuliwe zidi yake haraka iwezekanavyo. huyu jamaa yuko hatarini kuwatia matatizoni nyie wote wenye blog zenye mambo mazuri kama mfano hakingowi,kadidi, jiachie,tzuk na blog,mjengwa na nyingine nyingi tu.huyu jamaa amekua anaweka picha kwenye hata blog zenu halafu anaziweka kwake za watu bila idhini za wenyenazo na hana haki ya hizo picha ,amekua anahusika ubadilishaji wa picha za watu na kuwaonyesha wakiwa watupu,huyu jamaaa,amekua anawacha watu watukanwe na kwa vitendo kama hivyo polisi wanaommba msaada wa wananchi waishio tanzania kumuweka hadharani ili achukuliwe hatua endapo hata toa picha za watu wote kwenye blog hiyo ya kipuuzi.

Kwa upande wa watanzania waishio Marekani na U.k nao wanaendelea na uchunguzi wao maana watanzania waishio hizo pande mibli za dunia ndio wamekua saana wanawekwa kwenye hiyo blog kwa ajili tu ya kukashifu watu wasio hata wafahamu.tunaomba msaada wako tumtoe huyu mtanzania asie kua na heshima kwa jamii ya kitanzania.kwa kuweka upuuzi wake tayari kuna ndoa zimevunjika na zingine zikiwa na migogoro mikubwa hivi sasa
tunaomba msaada wako na utuwekee tangazo hili
mwenye taarifa yeyote kuhusina na swala hili wasiliana nasi Tanzania.dodoma300@gmail.com

No comments: