Wednesday, August 27, 2008

Ujenzi wa Daraja la Mbagala
Unaendelea..
Picha hii iliyopigwa na Mdau Badi Yusufu inaonyesha tundu pekee lililobaki kutolea maji upande wa pili katika njia ya mchepuko kuelekea Mbagala jijini Dar es Salaam,huo weusi wa maji ni kemikali kutoka kiwanda cha jirani.hufikiria kwamba wana mazingira hawapo wangelikuwepo tungeliendelea kula kambale kutoka katika bonde hili ambalo ni mkondo wa bahari.
-----
Ujenzi wa daraja kubwa katika mto Kizinga linalounganisha wakazi wa Mbagala na Mtoni katika barabara ya Kilwa umeanza jana na taarifa za wajenzi,daraja hilo litachukua miezi mitatu kukamilika.

Ili kuwezesha magari kuendelea na safari katika barabara hiyo muhimu na ya pekee kuingia Mbagala zote na kuelekea Kusini njia ya pembeni imetengenezwa ikiwa na kalvati moja tu tena dogo kama unavyoliona Pichani.
Watumiaji wa barabara hiyo wenye uzoefu wa zaidi ya miaka kumi wameelezea hofu yao ya kutengwa na mji iwapo mvua za vuli zitanyesha kutokana na wajenzi kuacha njia ndogo ya kutolea maji kama inavyoonekana.
Wanasema wakati wa mvua eneo hili la Mto Kizinga na bonde lake hufurika kuanzia upande wa msikitini hadi eneo ambalo linatumiwa na watu wa kijiwe kuoshea magari makubwa.
Wenyewe walipohojiwa walisema hali ya hewa kwa sasa itawawezesha kujenga daraja husika na kulimaliza kabla ya mvua za mwishoni mwa mwaka.Habari hii kwa Msaada wa Mdau Msimbe Lukwangule.

No comments: