Friday, August 22, 2008

Wale waliorudisha Fedha za
EPA nao Wachukuliwe Hatua
Kali-Malya
Na Bernard Rwebangira.
Baadhi ya wananchi hawajaridhika na hatua zilizochukuliwa na serikali juu wizi wa fedha za akaunti ya malipo ya nje maalufu kama EPA ya watuhumiwa kupewa hadi oktoba 31 kuwa wamerudisha hela hizo la sivyo watafikishwa mahakamani.
Mkurugenzi wa Mtandao wa jinsia nchini Bi Ussu Malya(Pichani)pamoja na baadhi ya wananchi wanaendelea kuhoji uhalali kwa watuhumiwa kupelekwa mahakamani iwapo watashindwa kurudisha pesa hizo na kuhoji je wale ambao wamerudisha hela hizo kama Rais Jakaya Kikwete alivyosema jana wakati analihutubia Bunge mjini dodoma ni basi watakua huru au? "Yaani mtu unaiba mabilioni ya umma kwa hati za kufoji kisha unashitukiwa na unaambiwa urudishe basi? hii haiingii akilini hata kidogo tunataka hatua zaidi" alimalizia Bi Malya na kuomba serikali kuchukua hatua zaidi.

No comments: