Rais wa Comoro Kulihutubia
Bunge...

Mh.Sambi,ambaye ataambatana na mwenyeji wake Rais Jakaya Kikwete,atalihutubia Bunge mara tu bada ya kipindi cha maswali na majibu milango ya saa nne unusu.
Rais huyo wa Comoros anatarajiwa, pamoja na mambo mengine,kutoa shukurani zake na za wananchi wake kwa Tanzania kwa kuongoza jeshi la Umoja wa Afrika katika mapambano yaliyofanikisha kuung'oa utawala wa kanali Mohammed Bacar katika visiwa vya Anjuani mapema mwaka huu.
Baada ya mgeni huyu kuondoka,Bunge litaendelea kujadili hotuba ya bajeti ya makadirio ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa ambapo Waziri Mh.Bernand Membe anatarajiwa kuhitimisha baadaye jioni.
No comments:
Post a Comment