Wednesday, August 27, 2008

Kampuni ya Zain Yatanua Huduma
Zake Vijijini..
Na Mwandishi Wetu.
KAMPUNI ya simu za mkononi ya Zain Tanzania ambayo sasa ni sehemu ya Mtandao unaotambulika duniani wa Zain Group,inaendelea kusambaza huduma zake katika maeneo mengi zaidi ya vijijini,ikiwa ni sehemu ya kutekeleza kauli mbiu yake ya A Wonderful World (Ulimwengu Maridhawa).
Katika mahojiano maalumu Dar es Salaam Leo kwenye ofisi za makao makuu ya Zain Tanzania,Ofisa Mkuu wa Biashara wa Zain Tanzania,Bw.Chiruyi Walingo alisema Zain inayoongoza kwa kusambaa maeneo mengi zaidi nchini,inapanua mtandao wake wa simu ili kuwafikia watu wengi zaidi nchini na hasa maeneo ya vijijini ili ziweze kuwafikia Watanzania Zaidi.

''Zain inaamini kwamba mawasiliano thabiti ni sehemu moja ambayo kampuni inaweza kutoa mchango mkubwa kwa jamii"alisema Walingo.

Alieleza kuwa kampuni imepania kuboresha huduma za mawasiliano maeneo ya vijijini,kwani ndio chachu ya maendeleo na kwamba inaendelea na juhudi za kujitangaza katika mikoa yote Tanzania.

Alitaja baadhi ya sehemu ambazo Zain Tanzania ndio mtandao pekee wa simu unaofanya kazi kuwa ni pamoja na Namuhula,Nyasamo,Nyangili,Misasi,Mbarika,Sumve,Maligisu,Kisorya, Kanguguli na Kadashi,Kanda ya Ziwa.

"Zain sasa ni sehemu ya mtandao wa dunia na azma yake ni kuwa moja ya kundi la kampuni kumi bora zinazoongoza katika simu za mkononi duniani hadi kufikia mwaka 2011”aliongeza kusema Walingo.

Aliongeza kusema kuwa mtandao wa mawasiliano wa kampuni hiyo unawafikia mamilioni ya wateja katika nchi 22 barani Afrika na Mashariki ya Kati kwa gharama nafuu.Pia alisema Zain ina mpango wa kupanua wigo wa huduma yake ya Mtandao Mmoja‘One Network’katika nchi zote inazotoa huduma Afrika,ili kuwawezesha wateja kuvuka mipaka ya kijiografia bila kurandaranda kutafuta mawasiliano na bila kulipia huduma ya simu zinazoingia.

Alifafanua kuwa kauli mbiu ya Zain ya ‘A Wonderful World’(Ulimwengu Maridhawa),inatoa nguvu,msukumo na kubadili uelekeo wa waajiriwa,wateja,washirika na wadau.

No comments: