Vodacom Miss Tanzania 2008 Nasreem
akabidhiwa gari Lake.


----
jana asubuhi kampuni ya simu ya mikononi iliyodhamini shindano la miss Tanzania 2008,Vodacom imekabidhi rasmi zawadi ya gari kwa mrembo wa Vodacom Miss Tanzania 2008 Nasreem Kalim.
Gari hilo jipya aina ya Suzuki Garnd Vitara lenye thamani ya sh Millioni 42 limekabidhiwa kwa mrembo huyo na meneja na meneja udhamini wa Vodacom Tanzania,Emillian Rwejuna.Makabidhiano hayo yamefanyika leo asubuhi katika ofisi za Vodashop zilizopo mtaa wa samora jijini Dar na kushuhudiwa na maofisa wa Baraza la sanaaa,Kampuni ya LINO ambao ndio wanaadaaji wa shindano hilo,wadau wa sanaa na waandishi wa habari.
Akizungumza muda mfupi baada ya makabidhiano hayo,Rwejuna alisema Vodacom Tanzania,itaendelea kuboresha zawadi kila mwaka kwa washindi na washiriki,amesema kuwa ni matumaini ya Vodacom Tanzania kwamba zawadi hiyo ya gari ambayo amekabidhiwa itasaidia kurahisisha utendaji na shughuli mbalimbali za kijamii za mrembo huyo.
Rwejuna amesema kuwa sehemu wajibu wa Vodacom Miss Tanzania ni kushiriki katika shughuli mbalimbali za kijamii,shughuli ambazo kwa kiwango kikubwa zina mlazimu kusafiri,hivyo ni muhimu sana kuhakikisha kwamba Vodacom Miss Tanzania anakuwa na usafiri wa kuaminika
No comments:
Post a Comment