Friday, August 22, 2008

Rais Kikwete akinguruma Bungeni
Mjini Dodoma Jana..



Rais Rais,Jakaya Kikwete akilihutubia Bunge Mjini Dodoma jana.Kulia ni Makamu wa Rais
Dr.Ali Mohammed Shein na wa pili kulia ni Spika wa Bunge Samwel Sitta.
----------------
Rais Jakaya Kikwete jana ametoa hotuba ndefu kwa masaa kama matatu hivi iliyogusa maeneo nyeti mbalimbali,hapo chini ni sehemu tu ya hotuba hiyo..
Rais Jakaya Kikwete amesema mengi kuhusu utawala bora,nidhamu na maisha lakini muungano tu ndicho ambacho nakiona amekiongelea kwa kutumia diplomasia sana na kusema watu wasikoroge mambo zaidi waache taasisi husika ziangalie kama kweli kuna kero katika muungano. Jambo jingine nishani za Comoro kwa askari na washiriki wengine.

Jambo jingine anataka uhuru wa sasa utumike unavyostahili,tuzoee kitu cha kusema watu na kuandamana lakini si kwa kuvuruga nchi.Uchochezi na habari za kuleta machafuko hazikubaliki. Ametoa fursa ya utamaduni wa kutoa maoni tusiutumie vibaya uhuru huo.Wananchi wanatakiwa kutumia vyema haki na fursa hiyo,Haki isiyokuwa na wajibu ni upuuzi mtupu.

.KUHUSU EPA
"Kuhusu EPA...,Agosti 18 nilipokea ripoti kutoka katika timu niliyounda,nimeipitia,lakini kuna mambo nimeagiza,moja ni kwamba wote waliopata fedha hizo wawe wamelipa ifikapo Oktoba 31,vinginevyo watakiona cha moto ni mahakamani tu,"alionya na kuongeza.

"Msione ma-gentle men wanapita mitaani wamefunga tai,tayari wengine tumewafilisi,tayari magari,hati za kusafiria na hata nyumba zao zimekamatwa,matajiri wa EPA wana hali mbaya kweli".
Rais Jakaya Kikwete amesena ni shs bilion 53 tu ndo zimerudishwa mpaka sasa.Watuhumiwa wa fedha hizo pamoja na kurudisha pesa wameporwa hati zao za kusafiria na kuwa watataifishiwa mali zao zote pamoja na magari yao ya kifahari waliokuwa wakitanulia nayo mitaani.
*Rais Kikwete amekiri kwamba pesa za EPA hazikuwa za serikali na kuwa ni za wafanyabiashara wa nje na kuwa baada ya kurudishwa zitaelekezwa kwenye kilimo lengo likiwa kuanzisha benki ya kilimo kwa mabenki wanasema kuwa kilimo hakikopesheki.

*Rais Jakaya Kikwete amezungumza mengi pamoja na kutoa ujumbe mzito katika masuala muhimu yanayohusu taifa kwa sasa.masuala hayo ni ya siasa,uchumi na jamii katika hili akagusia soka na haja ya TFF kuanza kujiandaa kuwa na mwalimu wao mwenyewe.

Rais Pia amezungumzia kazi zilizofanyika na kutoa mwelekeo wa baadaye na kusisitiza kuwa tunajenga nyumba tusigombee fito.

.KUHUSU ZANZIBAR

Rais Kikwete alisema haelewi mantiki ya mjadala huo kuendelea ukiwahusisha hata viongozi wa serikali kwani haamini kama kweli wanaouendeleza hawafahamu jambo hilo.
"Hivi kweli Watanzania tangu miaka 44 ya Muungano bado tunashindwa kuelewa kwamba zilizokuwa nchi mbili huru,Zanzibar na Tanganyika, ziliungana na kuunda nchi moja ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania?"alihoji Rais Kikwete aliyeonekana kukunja uso.

Alisema hadhi ya Zanzibar kuitwa nchi,ilikoma baada ya muungano kati yake na Tanganyika na kuunda nchi mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo ndio inayowatambulisha Watanganyika na Wazanzibari mbele ya mataifa mengine.

.SPIKA SITTA AMTAHADHARISHA RAIS KIKWETE.

Baada ya Rais jakaya Kikwete kumaliza kutoka hotuba yake jana bungeni mjini Dodoma

Spika wa bunge la jamhuri la Muuungano wa Tanzania Mh Samwel Sitta alimkumbusha Rais Kikwete kwamba kuwa ni makosa kusimamia haki za binadamu kwa wahujumu uchumi.

Mheshimiwa Spika Samwel Sitta alimtaka Rais Kikwete kuongeza ukali kidogo katika masuala ya rushwa na ufisadi na kwamba Bunge litasaidia kuiweka nchi sawa.

"Hongera sana mheshimiwa Rais,umetoa hotuba nzuri,tumesikia, kuna mambo ya msingi, kuna hili la utawala bora,ukiongeza ukali kidogo basi sisi wabunge tutakusaidia.Lakini,wakati mwingine haya mambo ya kuweka visingizio vya haki za binadamu kwa wahujumu uchumi, yanakwamisha maendeleo ya nchi,"alisema Sitta huku Rais akitabasamu.

Spika Sitta alifafanua kwamba, wakati mwingine kushindwa kushughulikia wahujumu uchumi kwa kisingizio cha haki za binadamu hurudisha nyuma maendeleo ya nchi.

*Wadau muda mchache ujao tutawaletea hotuba yote ya Rais Jakaya Mrisho Kikwete aliyohutubia jana mjini Dodoma.

Labels: Hotuba ya Rais Jakaya Kikwete Bungeni leo mjini Dodoma.Na Msimbe Lukwangule

No comments: