Wednesday, August 27, 2008

Tanzania Nchi ya Pili Duniani
Kwa utozaji Mkubwa wa Kodi Za
Mawasiliano..
Naibu Waziri wa Wizara ya Mawasiliano,Sayansi na Teknolojia,
Dk.Maua Daftari.
---
Tanzania ni nchi ya pili duniani kwa utozaji mkubwa wa kodi za mawasiliano,ambapo inatoza gharama ya asilimia 30 ukilinganisha na Uturuki ambayo ni ya kwanza kwa asilimia 45.Viwango hivyo ni vikubwa,na kwa upande wa hata nchini gharama hizo ni kubwa na zinaonekana kuwafaidisha zaidi kampuni za simu.
Hiyo yote inatokana na nchi kutokuwa na mkongo wake wa mawasiliano ambayo ungesaidia kupunguza gharama hizo na kuwabana wenye kampuni za simu ambao hutumia minara yao binafsi.Hivi karibuni Waziri wa Wizara ya Mawasiliano,Sayansi na Teknolojia,Profesa Peter Msolla aliwasilisha bungeni makadirio ya bajeti ya wizara yake kwa mwaka 2008/09 ambayo ilisisitiza pia ujenzi wa mkongo huo.
Mkongo wa mawasiliano wa Taifa ambao uko mbioni kujengwa,utasaidia kupunguza gharama za mawasiliano nchini zinazopanda mara kwa mara.Profesa Msolla anasema mara ukamilikapo ujenzi huo,itakuwa rahisi kwa Mamlaka ya mawasiliano kuwa na sababu za kuwabana kampuni binafsi za simu kupunguza gharama za mawasiliano kuliko ilivyo sasa.Habari hii na Ikunda Erick

No comments: