Tuesday, August 19, 2008

Rais Kikwete kulihutubia
Bunge Alhamisi...
--------------------
Rais Jakaya Kikwete keshokutwa atahutubia Bunge kwa mara ya pili tangu ashike uongozi wa nchi.Akitangaza mabadiliko ya ratiba za Bunge,Naibu Spika wa Bunge,Anne Makinda alisema Rais Kikwete atalihutubia siku hiyo katika Mkutano wake wa 12 ulioanza Juni 10 mwaka huu. Hiyo itakuwa ni mara ya pili kwa Rais Kikwete kulihutubia Bunge,alifanya hivyo kwa mara ya kwanza Desemba 30,2005,siku tisa tangu ale kiapo cha kushika madaraka ya Serikali ya Awamu ya Nne.
Taarifa zinaeleza kuwa Rais aliomba kulihutubia Bunge na Kamati ya Uongozi ya Bunge ilikaa mwishoni mwa wiki mjini hapa kujadili ombi la Rais na kulikubali.Kwa mujibu wa Naibu Spika, baada ya Rais Kikwete kulihutubia Bunge keshokutwa,Jumatatu ijayo,Rais wa Comoro,Ahmed Abdallah Sambi naye atalihutubia Bunge.
Naibu Spika alisema jana jioni Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa ilitarajiwa kuwasilisha makadirio ya matumizi ya fedha ya Wizara kwa mwaka huu wa fedha ambayo yatajadiliwa hadi leo asubuhi

No comments: