DC Tambarare..

Hello there.Kila niwezapo ntaleta"uwiano"wa picha na taswira mbalimbali nizinyakazo kuweka bayana kile ambacho wengi wameshindwa kukitambua juu ya upande wa pili.Japo wengi hudhani kila sehemu ndani ya nchi kama Marekani ni safi na yenye hadhi ya juu,tazama baadhi ya taswira za baadhi ya sehemu zenye wakazi wengi weusi na wenye kipato cha kati na chini.
Hapo ni maeneo ya NorthEast ambayo pia si ya kimaskini zaidi hapa DC.Lakini haya ni makazi ambamo watu wanaishi na kuna hizo"flats"ama appartments ambazo pia zimejaa watu waliopangisha. Lakini unaweza kuona hayo madirisha yamewekewa nondo na si kwa urembo kama tufanyavyo nyumbani, bali dalili ya"dokoadokoa"Kama nionavyo taswira zioneshavyo "bongo tambarare",si vibaya nami nikasema "DC tambarare"
No comments:
Post a Comment