Ujenzi wa Daraja la  Mbagala
 Unaendelea..
  -----
 Ujenzi wa daraja kubwa katika mto Kizinga linalounganisha  wakazi wa Mbagala na Mtoni katika barabara ya Kilwa umeanza jana na taarifa za  wajenzi,daraja hilo litachukua miezi mitatu kukamilika. 
 Ili kuwezesha magari kuendelea na safari katika barabara hiyo muhimu na ya pekee kuingia Mbagala zote na kuelekea Kusini njia ya pembeni imetengenezwa ikiwa na kalvati moja tu tena dogo kama unavyoliona Pichani.
Watumiaji wa barabara hiyo wenye uzoefu wa zaidi ya miaka kumi  wameelezea hofu yao ya kutengwa na mji iwapo mvua za vuli zitanyesha kutokana na  wajenzi kuacha njia ndogo ya kutolea maji kama inavyoonekana.
  Wanasema wakati wa mvua eneo hili la Mto Kizinga na bonde lake  hufurika kuanzia upande wa msikitini hadi eneo ambalo linatumiwa na watu wa  kijiwe kuoshea magari makubwa.
Wenyewe walipohojiwa walisema hali ya hewa kwa sasa itawawezesha kujenga daraja husika na kulimaliza kabla ya mvua za mwishoni mwa mwaka.Habari hii kwa Msaada wa Mdau Msimbe Lukwangule.
 Wenyewe walipohojiwa walisema hali ya hewa kwa sasa itawawezesha kujenga daraja husika na kulimaliza kabla ya mvua za mwishoni mwa mwaka.Habari hii kwa Msaada wa Mdau Msimbe Lukwangule.
No comments:
Post a Comment