Ajali ya Morogoro....
Basi la aina ya Scania T 820 AGE,Mali ya Simba Mtoto,likiwa limegongwa sehmu ya Dereva na kusababisha Dereva,Amri Masimba na Abiria Mary Chatahika,ambaye ni mchungaji wa kanisa la Asembles of God kufariki dunia papo hapo,Basi hilo lilogongwa na Lori T 680 AAB aina ya Scania lenye tella T 626 AAB ambapo Dereva wake,Aboud Hassan naye alifariki dunia,ajali ilitokea eneo la Doma,Wilayani Mvomero,katika barabara kuu ya Iringa-Morogoro.
Basi hilo lilikuwa linatokea Lilongwe Malawi kwenda Nairobi Kenya na Lori lilikuwa linatoka Dar es Salaam kwenda Zambia.Picha na habari na Mdau John Nditi wa TSN/Morogoro
No comments:
Post a Comment