Wale waliorudisha Fedha  za
 EPA nao Wachukuliwe Hatua 
 Kali-Malya
   Na Bernard Rwebangira.
 Baadhi ya wananchi hawajaridhika na hatua zilizochukuliwa na  serikali juu wizi wa fedha za akaunti ya malipo ya nje maalufu kama EPA ya  watuhumiwa kupewa hadi oktoba 31 kuwa wamerudisha hela hizo la sivyo  watafikishwa mahakamani. 
  Mkurugenzi wa Mtandao wa jinsia nchini Bi Ussu  Malya(Pichani)pamoja na baadhi ya wananchi wanaendelea kuhoji uhalali kwa  watuhumiwa kupelekwa mahakamani iwapo watashindwa kurudisha pesa hizo na kuhoji  je wale ambao wamerudisha hela hizo kama Rais Jakaya Kikwete alivyosema jana  wakati analihutubia Bunge mjini dodoma ni basi watakua huru au? "Yaani mtu  unaiba mabilioni ya umma kwa hati za kufoji kisha unashitukiwa na unaambiwa  urudishe basi? hii haiingii akilini hata kidogo tunataka hatua zaidi" alimalizia  Bi Malya na kuomba serikali kuchukua hatua zaidi.
 
No comments:
Post a Comment