Adha na karaha za barabarani
 Hapa baada ya mshike wa hapa na pale ndio akatokea trafiki kama  unavyomuona pichani,akielekea kwenye ajari husika kuweka maambo sawa
Wajameni njiani kuna adha na karaha nyingi sana za kukatisha tamaa kama  kutakosekana umakini na ustaarabu hasa kwa hawa madereva wetu!,nayasema haya  kwani yametokea mwishoni mwa wiki wakati Mdau mmoja wa blog hii alipokuwa anakwenda zake Moshi, njiani maeneo ya msata hivi akakutana na  bonge la foleni kama hivi pichani, akajihisi kama vile yuko Dar,asubuhi  flani hivi anawahi kazini, akawa anajiuliza hali hii inakuwa vipi na  huku!,kumbe bwana Lori limeanguka na kuziba barabara, ilikuwa yapata kama  saa tano na ushehe hivi asubuhi, ebwenae shughuli ilikuwa pevu.Lakini kwa bahati  nzuri alitokea trafiki fasta na kuirekebisha ile hali na magari yakaanza  kutambaa kama kawa.
No comments:
Post a Comment